Mkoa wa Ruvuma unatarajia kupanda miche ya miti ya aina mbalimbali 1,290,000 hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Januari 2025.
Miti hiyo inapandwa katika maeneo mbalimbali katika Wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma.
Kulingana na ratiba ya upandaji miti ya mwezi Januari iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS,Katika Halmashauri ya Madaba kwenye mashamba yaliyoungua moto eneo la Wino na eneo la hospitali ya Madaba jumla ya miti 260,000 imepandwa.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea eneo la hifadhi ya Litenga miti 100,000 imepandwa na hifadhi ya Lihanje miti 150,000 imepandwa.
Wilayani Mbinga eneo la mgodi wa TANCOAL na migodi mingine 16 miti 160,000 imepandwa, milima ya Kihangimauka miti 100,000 imepandwa,shamba la miti Mbambi miti 110,000 na milima ya Liumbe imepandwa miti 55,000.
Zoezi la upandaji miti pia limefanyika wilayani Nyasa katika eneo la Upolo ambapo miche 110,000 imepandwa na miche 15,000 imepandwa katika barabara za Kilosa na eneo la hospitali ya Wilaya.
Upandaji miti pia unatarajia kufanyika katika wilaya ya Namtumbo eneo la chanzo cha Mto Luegu ambapo miche ya miti 10,000 inatarajia kupandwa na wilayani Tunduru jumla ya miti 100,000 itapandwa katika shamba la miti la Halmashauri na maeneo ya sekondari za Tunduru na Masonya.
Uzinduzi wa upandaji miti kimkoa ulifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed katika viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma eneo la Mwenge mshindo Manispaa ya Songea ambapo Zaidi ya miti milioni 6.9 inatarajiwa kupandwa katika Mkoa mzima msimu huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.