• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MIKOA ya Ruvuma na Lindi yapewa mafunzo ya afya moja

Imewekwa kuanzia tarehe: August 16th, 2022

Asilimia 70 ya magonjwa ya binadamu yanatoka kwa wanyama

Mafunzo ya Timu za Afya Moja za utayari wa kukabiliana na  dharura za milipuko ya magonjwa yamefunguliwa mjini Mtwara.

Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yanafanyika kwenye kumbi wa Hotel ya Tiffany, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Wataalamu wanaopata mafunzo hayo ni maafisa maliasili,mifugo,wanyamapori,watalaam wa mazingira,madaktari wa binadamu na wanahabari kutoka wilaya za Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi na wilaya za Nyasa na Namtumbo mkoani Ruvuma.

Akizungumza kabla ya kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu  Meja Jenarali Michael Mumanga  ameitaja dhana ya afya moja inakutanisha watalaam na wadau kutoka sekta mbalimbali husasan sekta ya afya ya binadamu,Wanyama,kilimo na mazingira ili kutekeleza usalama wa afya moja duniani.

“Dhana ya afya moja inatumika zaidi  kwa sababu vimelea vingi vinavyosababisha vimelea vya magonjwa kwa binadamu vinatoka kwa Wanyama,maambukizi haya hutokea binadamu anapoingilia makazi ya Wanyama bila tahadhari’’,alisisitiza Meja Jenarali  Mumanga.

Hata hivyo amesema katika nchi za Afrika hali ni hatarishi zaidi kwa sababu zina mapori makubwa ambayo yanakaribiana na makazi ya watu mfano Bonde la Kongo ni kitovu cha magonjwa ya milipuko kama ebola na  homa ya bonde la ufa.

Amesisitiza kuwa ushirikiano wa watalaam katika afya moja hivi sasa ni ajenda ya dunia nzima kwa sababu inapunguza gharama katika kushughulikia  matishio ya magonjwa ya milipuko na vimelea mbalimbali vinavyoweza kutoka kwa Wanyama na kwenda kwa binadamu.

Kwa upande wake Dr.Vayan Laizer Mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza kwenye mafunzo hayo amelitaja lengo la mafunzo ya afya moja kuwa ni kuimarisha uelewa wa kila mdau na kujenga timu moja ili kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi na vimelea vya maradhi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo na kwa kutumia rasilimali chache zilizopo ni vema kufanyakazi kama timu ili kukabiliana na magonjwa yanayotoka kwa Wanyama.

“Kama tunavyojua zaidi ya asilimia 70 ya magonjwa yanayoambukiza binadamu yanatoka kwa Wanyama,hivyo tunatumia mwamvuli wa afya moja ili kujenga uelewa wa kila mmoja na hatimaye kupunguza athari kwa jamii na kuhakikisha binadamu anakuwa salama’’,alisisitiza Dr.Laizer.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Stella Kiambi alisema afya moja inajumuisha watalaam wa afya ya binadamu,wanyama wa porini na wanaofungwa na mazingira kwa ujumla kufanya kazi pamoja na kwamba kila mmoja kutekeleza majukumu yake kulingana na taaluma yake.

Dr.Mary Kitambi ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya,akizungumza kwenye mafunzo hayo amesisitiza ni vema kuzuia magonjwa kutoka kwa Wanyama kwa kutumia afya moja ambapo amesema serikali imeamua kuwaleta wataalam  Pamoja ili kujenga uelewa na kuwasiliana kukabiliana na dharura za milipuko ya magonjwa.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Agosti 15,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.