WANANCHI wa kata ya Mchoteka na Marumba wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wameishukuru serikali kwa kukamilisha ujenzi wa barabara inayounganisha vijiji mbalimbali katika kata hizo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema ,kukamilika kwa barabara ya Mchoteka-Masuguru-Marumba kwa kiwango cha Changarawe kumemaliza changamoto ya muda mrefu ya kukosa mawasiliano kati ya kata hizo mbili na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Matola Mohamed mkazi wa kijiji cha Masuguru amesema ,uthubutu uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita kujenga barabara hiyo ni kati ya mambo mazuri yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo ya kata hizo na wilaya ya Tunduru kwa ujumla.
Hassan Majongo,ameipongeza serikali kupitia Wakala wa barabara za mjini na vijijini(TARURA) wilaya na mkoa kujenga barabara hiyo kwa viwango vya hali ya juu kwani imesaidia sana kurahisisha mawasiliano na kupungua kwa ugumu ya maisha.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Tunduru Mhandisi Silvanus Ngonyani amesema barabara hiyo ,imejengwa kwa gharama ya Sh.milioni 265 zilizotokana na ongezeko la tozo zilizoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kiwango cha changarawe kwa km zote 17 na imefunguliwa rasmi baada ya kukamilika.
Amesema ,barabara hiyo ina faida nyingi kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara ikiwamo mpunga,mahindi,ufuta na korosho na muhimu kiulinzi wa nchi yetu kwa kuwa kata ya Mchoteka na Marumba zinapatikana na nchi Jirani ya Msumbiji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.