Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameidhinisha zaidi ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa tisa na vyoo vyenye matundu 16 katika Shule ya Msingi Mtelawamwahi, Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma.
Mradi huu unalenga kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundisha, pamoja na kuongeza nafasi za masomo kwa wanafunzi wa shule hiyo, ikiwemo wale wa madarasa ya awali
Timu ya wataalamu, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Ndugu Philemon Mwita Mgesa, ilitembelea eneo la ujenzi wa mradi huo.
Mkurugenzi aliwataka mafundi kuhakikisha wanakamilisha kazi haraka ili wanafunzi waanze kutumia madarasa mapya mara moja.
Juhudi hizi zinaendana na mkakati wa serikali wa kuboresha miundombinu ya elimu nchini, ambapo Rais Samia ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya na ukarabati wa shule zilizopo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.