Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Stephen Ndaki imetembelea na kukagua mradi wa kituo cha Afya kata ya Ligera Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ambapo serikali imetoa shilingi milioni 500 kutekeleza mradi huo.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho MGANGA Mfawidhi wa Zahanati ya Ligera Abel Gadson amesema kati ya fedha zilizotolewa hadi sasa zimetumika shilingi milioni 451.35.
Ameyataja majengo yaliyojengwa kuwa maabara,jengo la wagonjwa wa nje,jengo la upasuaji,wodi ya wazazi,jengo la kufulia na kuchomea taka
Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma imeipongeza Kamati ya Ujenzi kwa kusimamia vizuri mradi huo na kuwaagiza kufanya marekebisho kwenye framu na maeneo mengine yenye dosari ili mradi huo uanze kuwahudumia wananchi wa kata ya Ligera yenye vijiji vitano ambavyo ni Mtelawamwahi,Njomlole,Namahoka,Muungano na Ligera.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.