HALMASHAURI ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma,imetenga Sh.milioni 62,500,000 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha zao la ufuta na soya katika msimu wa kilimo 2024/2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Philimon Magessa amesema,fedha hizo zitatumika kuwajengea uwezo maafisa ugani na wakulima kama mpango wa Halmashauri wa kuimarisha na kuongeza vyanzo vyake vya mapato.
Amesema,kupitia mpango huo Hamashauri imehamasisha wananchi umuhimu wa kilimo cha zao la ufuta kwa kugawa mbegu bora kwa wakulima ili kuwavutia kulima zaidi zao hilo ambalo limeonesha mafanikio makubwa.
Kwa mujibu wa Magessa,hatua hiyo itasaidia wilaya ya Namtumbo kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara na Halmashauri kupata mapato na kukidhi mahitaji muhimu ya uendeshaji wa Halmashauri.
Amesema,kwa kuzingatia ukubwa wa eneo na uwezo wa ardhi kuzalisha mazao ya biashara Halmashauri imejipanga kuwekeza kwenye kilimo(block Farmina)kwa mazao ya Soya na Ufuta.
Ameutaja,mkakati uliopo ni kupima maeneo na kuyagawa kwa wawekezaji wazawa na wageni kwa matarajio ya kukusanya ushuru wa mazao na maeneo hayo ni Limamu ekari lenye 17,000,Ligera,Mchomoro na Likuyu.
Amesema,wameweka mikakati ya kuongeza mapato yake ya ndani ikiwemo kuhuisha na kuvijengea uwezo vyanzo vya mapato vilivyopo ili viweze kufanya vizuri zaidi.
Ameitaja mikakati hiyo ni pamoja kufanya ukarabati wmajengo yote yanayokodishwa,kuwajengea uwezo wakusanyaji wa mapato ili waweze kukusanya zaidi na kuajiri vibarua kwa ajili ya kukusanya mapato kwenye maeneo mbalimbali.
Amesema,watawajengea uwezo watendaji wa vijiji na kata juu ya mbinu sahihi za kusimamia ukusanyaji wa mapato,kutunga na kusimamia sheria ndogo za ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo yatachangia asilimia 0.8 ya mapato ya sasa ya Halmashauri.
Magessa amesema,mkakati huo ulianza tangu mwaka 2027/2018 unatarajia kuiwezesha Halmashauri kukusanya na kufikia malengo kwa asilimia mia moja au zaidi ifikapo mwaka wa fedha 2029/2030.
Ameongeza kuwa,wataimarisha na kusimamia sekta ya uwekezaji hasa kwenye madini yanayopatikana na katika wilaya hiyo yakiwemo madini ya Uranium,Kwatz,Makaa ya mawe,Tantalaiti,Titaniam,Manganizi na Dhahabu.
Ameyataja madini mengine kuwa ni Nobiamu, Ulanga, Lithiamu,Beriliamu,Amazonaiti,Topazi ambapo kampuni ya Mantra inafanya utafiti wa madini ya Urani katika kijiji cha Amani,kata ya Magazini na kutoka chanzo hicho Halmashauri inatarajia kupata wastani wa Sh.milioni 500.
Amekitaja,chanzo kingine ni kuuza hewa Ukaa kwa Kampuni ya Carbon Tanzania yenye makao makuu mjini Arusha ambayo imesaini mkataba na Halmashauri kwa kushirikiana na Jumuiya za hifadhi maliasili kwa jamii.
Amezitaja jumuiya hizo kuwa ni Kipalang’andu,Kimbanda na Kisungule ambapo Halmashauri itapata asilimia nane ya fedha zitakazotokana na mauzo ya kaboni na mapato yanayotarajiwa ni Sh.milioni 400.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.