HALMASHAURI ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imetenga shilingi milioni 69 kujenga kituo cha askari wanyamapori katika kijiji cha Nambecha ili kukabiliana na Wanyamapori.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya wakati anazungumza na wananchi wa kijiji cha Nambecha kufuatia malalamiko ya wakulima waliovamiwa na tembo kwenye mashamba yao.
Amesema kukamilika kwa jengo hilo kutaimarisha Usalama wa wananchi na mazao katika vijiji vyote ambavyo vipo karibu na hifadhi za Wanyamapori.
wananchi katika kijiji cha Nambecha wameiomba serikali kuongeza askari Wanyamapori ili kuongeza ulinzi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.