SERIKALI yatoa millioni 699 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Njoka lenye ukubwa wa mita 20 na ambalo litapitika muda wote na kusaidia kufungua barabara Muhukuru mpaka Kizuka itakayochochea uchumi kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katka Halmashauri ya wilaya ya Songea
“Barabara hii ni barabara muhimu, ni barabara ya huduma ni barabara ya uchumi ni barabara itakayoimarisha ulinzi,” na kipekee ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja alisema Waziri Mhagama.
Waziri Mhagama alifafanua, serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga daraja la mto Mgugusi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili madaraja yote makubwa yaweze kupitika katika majira yote ya mwaka wakati wa mvua na wakati wa kiangazi.
Aidha ujenzi wa madaraja madogo madogo manne umekamilika na wakala wa barabara vijijini TARURA wanamalizia ujenzi wa madaraja mengine manne madogo madogo yaliyobakia katika ujenzi wa barabara.
“Ukamilishwaji wa ujenzi wa barabara utarahisishia wananchi kupata huduma ya usafiri kwa haraka na kuchochea ukuaji wa Miji,” alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mhe. Menas Komba amesema ujenzi wa daraja hilo utasaidia serikali kuongeza mapato katika mazao ya bishara na chakula.
“Barabara inaenda kuwakomboa wakulima wa wilaya ya Songea kwa kurahisisha huduma ya usafiri, na tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kwa kusimamia vizuri ilani”
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Songea Vijijini Ndg. Thomas Masolwa amempongeza Mhe. Rais kwa kutatua changamoto kwa wananchi, na kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Njoka.
Awali katika taarifa wakala wa barabara vijijini TARURA Mhandisi Johnson Kweka alisema Mkandarasi HERA Construction ameshatekeleza kazi za kusafisha eneo la daraja, kuondoa miti katika eneo la mradi, kuchimba udongo na kupasua mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa daraja.
Amefafanua kwamba Mkandarasi anaendelea na ufungaji wa nondo na boksi kwa ajili ya ufungaji wa nguzo na mikono ya daraja na ujenzi umefika asilimia 40
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.