Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imepokea shilingi milioni 893 kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na ujenzi wa shule mpya kupitia mradi wa kuboresha miundombinu ya shule za msingi BOOST;
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile amekagua utekelezaji wa miradi hiyo ambapo amewataka wataalam hao kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.
Mheshimiwa Ndile amewataka Walimu wakuu na Maafisa watendaji kusimamia miradi ya BOOST na kuhakikisha inakamilika ifikapo Juni 30 2023.
Mradi wa BOOST katika Manispaa ya Songea unajengwa shule saba za Msingi kwa lengo la kuboresha miundo mbinu ya kusomea na kujifunzia ya Elimu Msingi na awali.
Mradi wa BOOST katika Manispaa hiyo unatekelezwa katika shule za msingi Kipera, Mbulani,Ruhuwiko, Matogoro, Mkuzo,Amani, na Bombambili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.