• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MILIONI 950 kujenga vituo viwili vya afya Manispaa ya Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: November 29th, 2021

SERIKALI imetenga Sh.milioni 950 wa ajili ya kujenga vituo viwili vya Afya katika kata ya Msamala na Lilambo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, ikiwa ni mkakati wake wa kusogeza huduma za matibabu  kwa wananchi wa kata hizo.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt Frederick Sagamiko, wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo  cha Afya Msamala kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.

Alisema, kati ya fedha hizo Sh.milioni 500 zitatumika kujenga kituo cha afya Msamala na Sh.milioni 450 kwa ajili ya kujenga kituo cha afya Lilambo kata ya Lilambo.

Dr. Sagamiko alisema,mradi wa ujenzi wa kituo  cha Msamala umeibuliwa na wananchi wenyewe  kwa madhumuni ya kupunguza kero ya kutembea umbali mrefu hadi  kituo cha afya Mjimwema na Hospitali ya rufaa Songea kufuata matibabu.

Dr.Sagamiko alisema,ujenzi wa mradi huo utahusisha jengo la maabara,upasuaji,jengo la wagonjwa wa n je,wodi ya wanawake,choo cha nje,kichomeo taka,shimo la kondo na shimo la maji taka.

Kwa mujibu wa Dkt Sagamiko,katika utekelezaji wa mradi huo Serikali imetoa Sh.milioni 500 ambapo wananchi wa kata hiyo wamechangia kiasi cha Sh.milioni 2 na unatekelezwa kwa mfumo wa force akaunti  na umewezesha wananchi hasa wanaoishi kata hiyo kushiriki katika shughuli za ujenzi na kujipatia kipato.

Dr. Sagamiko alitaja  manufaa ya mradi huo mara utakapokamilika ni upatikanaji wa huduma bora ya mama na mtoto na hivyo kupunguza vifo vya akina mama na mtoto kutoka 202 hadi 190 kwa vifo 100,000 kwa mwaka.

Faida nyingine ni upatikanaji wa huduma ya dharura ya upasuaji kwa akina mama wajawazito,kupungua kwa magonjwa ya kuambukiza na yasioambukiza pamoja na wananchi watapa elimu ya lishe,hivyo kupunguza tatizo la utapiamlo kwa Watoto.

Aidha huduma nyingine zitakazo patikana ni chanjo,huduma ya tohara  huduma ya upimaji wa VVU/ukimwi na kuzuia maambukizi pamoja na kupunguza mzigo wa wagonjwa uliokuwa unaielemea Hospitali ya mkoa na kituo cha afya Mjimwema.

Pia alisema,  katika bajeti ya mwaka 2021/2022 Manispaa  hiyo imepanga kutumia Sh.450,000,000.00 ikiwa ni fedha za mapato ya ndani kujenga kituo cha Afya Lilambo na wananchi wamechangia Sh.3,295,000.00 ambapo Sh.160,000,000.00 zimetolewa kutekeleza kazi hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,amemtaka  fundi anayesimamia mradi huo kuhakikisha  unajengwa kwa viwango na unakamilika kwa wakati ili uweze kuleta tija kwa wananchi ambao walisubiri mradi huo kwa

Alisema,lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuwatatua kero wananchi zilizokuwepo ikiwemo huduma  za matibabu,ambapo amewapongeza wananchi wa kata ya Msamala kwa kuibua mradi huo na kushiriki katika shughuli za ujenzi.

Brigedia Jenerali Ibuge alisema,Serikali ya mkoa itakuwa bega kwa bega na wananchi hao na kufuatilia kwa karibu  mradi huo ili ukamilike haraka.

Diwani wa kata ya Msamala Michael Mbano alisema, kata ya Msamala ni kubwa na yenye wakazi wengi,hata hivyo kwa muda mrefu haikuwa na huduma zozote za matibabu badala yake wananchi walilazimika kwenda  kutibiwa Hospitali ya mkoa na kituo cha Afya Mjimwema.Mbano ameishukuru Serikali  kutoa fedha za  ujenzi wa kituo hicho, kwani kitakapo kamilika  wananchi wa watapata matibabu karibu na kuwa  na afya njema itakayowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.