• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MIRADI ya kitaifa ya TANROADS inavyoufungua Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: March 17th, 2025

Uwanja wa Ndege Songea

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa mabilioni ya fedha kutekeleza miradi mbalimbali ya kitaifa katika Mkoa wa Ruvuma.

Uwanja wa Ndege wa Songea ni mojawapo ya miradi mikubwa ya kitaifa inayolenga kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga nchini.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi  Salehe Juma anasema Ujenzi wa uwanja huu ulianza Aprili 2019 na ulikamilika Disemba 2023 kwa gharama ya shilingi bilioni 38.139.

Anabainisha kuwa  Mradi huu ulitekelezwa na Mkandarasi China Henan International Cooperation Group Co. Ltd. chini ya usimamizi wa kampuni za uhandisi za Atkins Tanzania Ltd, Howard Humphreys na Advanced Engineering Solutions Limited.

Kukamilika kwa uwanja huu kunatarajiwa kuboresha huduma za usafiri wa anga na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

Barabara ya Likuyufusi-Mkayukayu

Juma anabainisha kuwa Mradi wa ujenzi wa barabara ya Likuyufusi-Mkayukayu unahusisha ujenzi wa kilometa 60 kwa kiwango cha lami. Hivi sasa, mradi huu uko katika hatua za mwisho za manunuzi baada ya mkandarasi wa awali kubainika kuwa hana uwezo wa kutekeleza kazi ipasavyo.

Hata hivyo Meneja wa TANROADS Mkoa anasema Serikali imehakikisha kuwa fidia kwa waathirika wa mradi imeshatolewa, ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi bilioni 5.2 kimetumika kwa malipo ya fidia.

Ujenzi wa barabara hii unatarajiwa kuongeza ufanisi wa usafiri na kurahisisha shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.

Barabara ya Songea-Rutukira na Songea Bypass

Huu ni mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya kilomita 116, ikijumuisha kilomita 16 za barabara ya mchepuko ya Songea (Songea Bypass).

Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unasimamiwa na wahandisi washauri wa kampuni za LEA International, LEA Associates na Howard and Humphrey.

Kwa mujibu wa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Hadi sasa, fidia ya shilingi milioni 646.964 imeshalipwa kwa waathirika wa mradi katika sehemu ya Songea - Lutukira, huku fidia kwa barabara ya mchepuko ya Songea bado ikisubiri taratibu za mwisho za malipo.

Kukamilika kwa mradi huu kutarahisisha usafiri na kupunguza msongamano wa magari mjini Songea.

Barabara ya Lumecha-Kilosa-Kidatu

Mradi huu unahusisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 435.8 kwa kiwango cha lami, ambayo itaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Morogoro.

Awali, mradi huu ulikuwa umepangwa kutekelezwa kwa mtindo wa Usanifu, Manunuzi, Ujenzi na Ufadhili, lakini sasa utafuata mtindo wa Sanifu na Jenga (Design and Build).

Mhandisi Juma anasema Ujenzi wa barabara hii unatarajiwa kuimarisha usafiri kati ya mikoa hiyo miwili na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa na abiria.

Miradi hii yote ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Kukamilika kwake kutakuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha usafiri, biashara na uwekezaji.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.