MISS Utalii Tanzania 2020 Ruvuma Fidea Hilary bado anaendelea kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Ruvuma kwa lengo la kuvitangaza ili kukaribisha wawekezaji.Miss utalii huyo ametembelea Pori la akiba la Liparamba ambalo lipo katika wilaya za Mbinga na Nyasa na kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika pori hilo lenye tembo wakimbizi wa nchi ya Msumbiji na simba weupe ambao wanavutia wengi.
Afisa Utalii wa Pori hilo Maajabu Mbogo amesema pori hilo ambalo limesheheni miti aina ya miyombo na wanyama wa aina mbalimbali lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kwamba pori hilo lina maporomoko ya Nakatuta kutoka mto Ruvuma ambayo yamekuwa kivutio adimu cha utalii Kulingana na Mbogo pori hilo lina ndege wa aina mbalimbali,maua na bustani ya mawe inayovutia watalii wengi na kwamba ukiwa ndani ya pori la Liparamba unaweza kufanya utalii wa kuruka ,kupiga kasia,kuogelea na kuvua samaki katika mito iliyipo ndani ya pori hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.