Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Innocent Bashungwa amesema watatembeza bakora kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya lami kutoka Amanimakoro hadi Ruanda wilayani Mbinga kuhakikisha anajenga barabara usiku na mchana kwa kuwa yupo nyuma kwa asilimia 75.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Amanimakoro na Ruanda Wilaya ya Mbinga na wananchi wa kijiji cha Lituhi Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,Bashungwa amesema serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 155 kujenga barabara ya lami kuanzia Kitai hadi bandari Ndumbi ziwa Nyasa.
Hata hivyo amemtaka Mkandarasi anayejenga kipande cha barabara ya Amanimakoro hadi Ruanda wilayani Mbinga chenye urefu wa kilometa 35 kukamilisha kazi hiyo ambayo mkataba wake umekwisha tangu Desemba 2023 na mradi upo asilimia 25 tu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema watambana koo Mkandaras huyo ili akamilishe kazi kwa kuwa serikali imewalipa zaidi ya shilingi bilioni 11 malipo ambayo ni makubwa kuliko kazi waliyoifanya.
Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 60 kujenga barabara ya lami kipande cha Amanimakoro hadi Ruanda chenye urefu wa kilometa 35 pia imetenga shilingi bilioni 96 kujenga barabara ya lami kipande cha Ruanda hadi Ndumbi chenye urefu wa kilometa 50.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.