SERIKALI kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA imesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji Kata ya Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.5.
Hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa kwa mwaka mmoja imefanyika katika kijiji cha Mtyangimbole ambapo mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema.
Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa Mkoa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali mkoani Ruvuma ukiwemo mradi huo wa maji Mtyangimbole.
Amewapongeza wananchi wa Mtysngimbole kuchangia shilingi milioni 19 kwenye mradi huo ambapo sasa serikali imeunga mkono juhudi za wananchi kwa kutoa mabilioni ya fedha kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuanza kuwanufaisha wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo amesema uwepo wa Rais mama hapa nchini umeongeza kiwango cha fedha za kutekeleza miradi ya maji nchini kwa zaidi ya asilimia 90.
“Kama kuna mtu anajua dhamira ya Mheshimiwa Rais kumtua mama ndoo kichwani ni sisi RUWASA kwa hiyo tuna ushahidi wa wazi kabisa wa kifedha unaotuwezesha kutekeleza miradi hii kwa ufanisi mkubwa “alisema Mhandisi Kivegalo.
Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amekitaja chanzo cha maji cha Mtyangimbole kuwa kina uwezo wa kuzalisha maji lita 1,883,562.16 kwa siku ambapo mahitaji ya wananchi ni lita 633,621.16
Mradi wa maji wa Mtyangimbole uliibuliwa na wananchi wa vijiji vya Mtyangimbole,Luhimba na Likalangilo .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.