• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma hauna shule inayoitwa Litapatile,taarifa za mtandaoni ni uzushi mtupu

Imewekwa kuanzia tarehe: April 23rd, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekanusha taarifa zilizosambaa mtandaoni zikidai katika Halmashauri ya Madaba kuna shule inayoitwa Litapatile ambayo wanafunzi wanasoma kwenye kibanda cha nyasi.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Aprili 22 mwaka huu,RC Ibuge amesema video hiyo inaonesha uwepo  wa wanafunzi,waliovalishwa sare za shule wakiwa katika kibanda cha miti ambacho msimuliaji anaita shule ikiwa na wanafunzi wanaodaiwa kusoma kuanzia darasa la Awali,kwanza,pili hadi la tatu.

Brigedia Jenerali Ibuge alibainisha Zaidi kuwa video hiyo inasimulia kuwa shule hiyo ina Mwalimu wa kujitolea anayedaiwa kulipwa na wazazi na kwamba wananchi hao wanatamani kusaidiwa kujengewa darasa la kusomea watoto wao.

“Ndugu wanahabari,ukweli ni kwamba hakuna shule inayoitwa  Litapatile katika Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma,chanzo cha taarifa hiyo ni uzushi’’.alisema.

RC Ibuge ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla kupuuzia  taarifa hiyo ambayo ina malengo binafsi ya kuhalalisha kosa la wazazi la  kuwanyima haki ya kusoma watoto wao.

Hata hivyo amesema wananchi wameacha kwa makusudi kuishi katika maeneo rasmi ya vijiji na vitongoji na kuamua kwenda kuishi porini umbali wa kilometa Zaidi ya 50 toka kijijini kwa kisingizio cha kufanya shughuli za uzalishaji mali ambazo ni kilimo na ufugaji.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameutaja msimamo wa serikali ni kwamba,watoto hao wanayo haki ya kupata elimu kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na kwamba wazazi wao wanawajibu wa kuhakikisha watoto wao wanaandikishwa na kuhudhuria masomo kwa mujibu wa taratibu.

“Pamoja na kuwepo utaratibu wa shule shikizi,bado shule hizo zina utaratibu wake wa kuanzishwa ikiwemo kuwepo na makazi rasmi ,kibanda hiki kipo porini,hakuna hata njia ya kufika huko kwa usafiri isipokuwa kwa miguu,shule shikizi inahitaji huduma za kielimu ili watoto wapate haki ya kupata elimu bora’’,alisisitiza Ibuge.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa shughuli zao haziathiri haki ya watoto wao kuandikishwa na kupata elimu.

Amesisitiza kuwa serikali  ya Mkoa  inaendelea kusimamia haki ya watoto kupata elimu kwa kutekeleza Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1976 inayolinda haki ya msingi ya watoto wote kupata elimu.

Ametahadharisha kuwa ni kosa kwa mzazi kutohakikisha kuwa mtoto wake anaendelea na shule hadi kufikia darasa la saba na kwamba mtu yeyote atakayesababisha mtoto wake asiendelee na shule atatiwa hatiani.

Amesisitiza kuwa serikali   haitamvumilia mzazi yeyote atakayefanya kwa makusudi kumnyima haki ya kupata elimu mtoto wake kwa kisingizio chochote ikiwemo kwenda kuishi porini kwa kisingizio cha kulima au kufuga.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Aprili 23,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.