Mkoa wa Ruvuma unaendelea kutoa udhibiti wa magonjwa kwa mifugo ikiwemo ng'ombe ,mbuzi ,kuku na mbwa.
Naye Afisa mifugo mkoa wa Ruvuma Nelson William, ameleeza mwezi Julai 2020 hadi machi 2021 magonjwa yaliyo jitokeza zaidi ni Ndigana kali,Ndigana baridi,Homa ya mapafu kwa ng'ombe na mbuzi,ugonjwa wa mapele ngozi,kideri na homa ya matumbo kwa kuku na ndui
"Ng'ombe wamepatiwa chanjo dhidi ya homa ya mapafu(CBPP), ng'ombe 500 dhidi ya ugonjwa wa midomo na miguu,50 dhidi ya ugonjwa wa Ndigana kali,157 dhidi ya ugonjwa wa kutupa mimba(Brucellosis) Mbuzi 1567 dhidi ya homa ya mapafu(CPPP) mbwa 6787 wamepewa chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa (Rabies) kuku 323,624 dhidi ya ugonjwa wa kideri,10606 dhidi ya ugonjwa wa ndui na 2386 dhidi ya ugonjwa wa Gumboro" alisema william.
Aidha ,alisema katika utekelezaji wa zoezi la uogeshaji wa mifugo michovyo 5,929 ya uogeshaji hufanyika kwa wiki sawa na michovyo 23,818 kwa mwezi ni sawa na michovyo 213,467 kwa kipindi cha mwezi Julai 2020 hadi Disemba 2021
alisema Matokeo ya uogeshaji Mkoa wa Ruvuma ni kupungua kwa vifo vya mifugo vitokanavyo na magonjwa yaenezwayo na kupe na Ndorobo.
"kwa sasa Mkoa unatekeleza ujenzi wa majosho 15 ,katika Halmashauri za Tunduru majosho 9, Songea DC majosho 5 na Nyasa josho moja" Alisema william
Hata hivyo Mkoa umeendelea kuhimiza Halmashauri kuweka mikakati ya kujenga majosho mapya kupitia mapato ya ndani.
William amesema pamoja na jitihada hizi katika zoezi la uogeshaji mifugo kuna changamoto ambazo ni pamoja na uchache wa mifugo inayiogeshwa kwa majosho mengi hivyo kupelekea ugumu wa uendeshaji wa majosho .
Imeandaliwa na Janeth Ndunguru
Kitengo cha mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.