MKOA wa Ruvuma Ufaulu wa kidato cha nne Mwaka 2020 /2021 umeongezeka kutoka asilimia 86.06 hadi kufikia asilimia 90.1.
Akitoa Taarifa hiyo Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Hakimu Mafuru amesema Mkoa unajumla ya Shule za Sekondari 218 zikiwemo 160 za Serikali na 58 ni Shule binafsi.
Amesema kati ya Shule hizo 160 za Serikali Shule tano ni za bweni na Shule 155 ni za kutwa kati ya Shule hizo zenye kidato cha Tano na Sita ni 35 za Serikali 23 na zisizo za Serikali 12.
Hata hivyo amesema hadi kufikia Machi 2022 mahitaji ya Walimu wa Shule za Sekondari ilikuwa 4,0441 wliokuwepo ni 3,523 na upungufu ulikuwa 518.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Juni 2022 ilitoa ajira kwa Walimu katika Mikoa yote ya Tanzania Mkoa wa Ruvuma Ulipangia jumla ya walimu 389”.
Amesema walimu hao walikuwa wanaume 279 na wanaume 110 kwa Shule za Msingi na Sekondari na walimu 213 walipangiwa katika Shule za Sekondari ambapo kati ya hao Walimu 212 walipangiwa katika Shule za Msingi na wamekwisha kulipo katika Shule walizopangiwa.
Afisa Elimu amesema hali ya Ufaulu kwa kidato cha nne Mkoa wa Ruvuma kitaaluma unaendelea kufanya jitihada za makusudi ili kuweza kupata matokeo mazuri Mwaka 2020 Mkoa ulikuwa na ufaulu wa asilimia 89.4 na Mwaka 2022 Mkoa umefaulu kwa asilimia 90.1.
Amesema Ufaulu kidato cha Sita Mwaka 2022 Mkoa umeendelea kufanya jitihada kuboresha ufaulu wa Wanafunzi katika Matokea katika kidato cha Sita na kufikia wastani wa asilimilia 99.9.
“Matokea ya Mtihani wa Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 hadi 2022 walifaulu kwa asilimi 99.7 hadi asilimia 100”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 12,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.