• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma kupandisha hadhi Hifadhi mbili kuwa mapori ya akiba

Imewekwa kuanzia tarehe: January 18th, 2023

MKOA wa Ruvuma umeridhia kupandisha hadi Hifadhi mbili za misitu kuwa mapori ya akiba (Game Reserve) kwa lengo la kuendeleza sekta ya maliasili na utalii.

Afisa Maliasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Africanus Challe ameyataja mapori hayo kuwa ni  Gesimasowa lililopo Madaba lenye ukubwa wa kilometa za mraba 764 na  pori la Litumbandyosi lililopo Mbinga lenye ukubwa wa kilometa za mraba 494.

Amayataja mapori hayo kuwa  ni Sehemu ekolojia ya Selous Niassa na kwamba  mpaka sasa bado mapori hayo hayajapata Tangazo la Serikali la kuwa na mapori ya akiba rasmi.

Kwa mujibu wa Afisa Maliasili huyo,Mkoa una mpango wa kuanzisha mashamba ya Wanyamapori (Wildlife Farms) katika Kisiwa cha Lundo ziwa Nyasa wilaya ya Nyasa pamoja na Chuo cha Maliasili cha Likuyusekamaganga wilayani Namtumbo ili wananchi waweze kujifunze kutoka mashamba ya wanyamapori ya serikali ili wao waweze kuanzisha mashamba binafsi ya wanyamapori.

Hata hivyo Challe amesema Mkoa wa Ruvuma unakabiliwa na changamoto kubwa ya Wanyamapori waharibifu hasa Tembo hivyo kuharibu mali na kuhatarisha maisha.

“kwa kipindi cha Miaka mitano iliyopita matukio ya Wanyamapori Waharibifu na wakali imekuwa ikiongezeka katika wilaya za Tunduru na Namtumbo hivyo kusababisha ongezeko la fedha za kifuta jasho na kifuta machozi zinazolipwa kwa jamii zilizoathirika’’,alisema.

 Kulingana na Afisa Maliasili huyo mwaka 2019/2020 jumla ya wananchi 1625 waliathirika na wanyamapori wakali na waharibifu dhidi ya mali na maisha ya binadamu.

Ameongeza kuwa katika kipindi hicho jumla ya ekari 2879.33 ziliharibiwa, wananchi wawili   walijeruhiwa na wananchi wanne waliuwawa na  wanyamapori.

Challe amebainisha zaidi kuwa  mwaka 2020/2021 jumla ya watu 435 waliathirika na wanyamapori na jumla ya ekari 2562.83 ziliharibiwa, watu saba waliowawa  na watu sita kujeruhiwa.

Hata hivyo amesema malipo ya fedha ya kifuta jasho na kifuta machozi yamefanyika katika Wilaya ya Tunduru ambapo takribani  shilingi milioni 270,650,000 zimelipwa kwa waathirika  katika kipindi cha mwaka 2020/2021 na mwaka 2019/2020.

Amesema licha ya jitihada zinazochukuliwa na Mkoa kukabiliana na wanyamapori waharibifu,Mkoa umependekeza  tembo waweze kurejeshwa kwenye makazi yao.

Amezitaja hatua nyingine za kukabiliana na wanyamapori waharibifu kuwa ni Wizara ya Maliasili na Utalii,TAWA,TANAPA kwa kushirikiana na Halmashauri kuanzisha vituo vya askari vya kudumu vya kudhibiti wanyamapori waharibifu kwenye maeneo korofi na kuziwezesha Halmashauri vitendea kazi kama mahema, gari na mafuta, Silaha, risasi na vilipuzi kwa ajili ya kupambana na wanyamapori waharibifu hususani tembo.

Amezitaja hatua nyingine kuwa ni Wizara kutenga bajeti au fedha kwa ajili ya kudhibiti wanyamapori waharibifu kwenye Wilaya zenye changamoto hasa Tunduru na Namtumbo.

Hatua nyingine amezitaja kuwa ni Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia ndege zisizo na rubani (drone) na  helcopter kuwaondoa Tembo katika maeneo jirani na makazi ikiwemo hifadhi ya msitu wa Mlima Kipiki wilayani Namtumbo.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 18,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.