Katika ulimwengu unaokimbia kwa kasi ya kiteknolojia, mwekezaji wa kisasa anatafuta zaidi ya ardhi na watu – anatafuta mazingira rafiki kwa biashara, fursa halisi zenye faida, na uthabiti wa miundombinu.
Mkoa wa Ruvuma, uliopo kusini mwa Tanzania, umeibuka kama eneo endelevu kwa uwekezaji wa kimkakati.
Kilimo – Sekta Isiyoisha Mvuto
Ruvuma ni “powerhouse” ya kilimo. Ardhi yake kubwa na yenye rutuba ina uwezo wa kuzalisha kila aina ya mazao – ya chakula kama mahindi, mpunga, maharage
Mazao ya biashara kama kahawa, korosho, na miwa. Zaidi ya hekta 197,000 zinafaa kwa umwagiliaji, lakini ni asilimia 3.7 tu iliyoendelezwa.
Hii ni nafasi ya dhahabu kwa kampuni au mwekezaji anayetafuta kujenga miradi ya kilimo cha umwagiliaji au greenhouse farming kwa soko la ndani na la nje.
Halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma zimetenga zaidi ya ekari 57,000 kwa ajili ya kilimo cha pamoja. Hii ni platform nzuri kwa wawekezaji wanaotafuta kushirikiana na wakulima wadogo kupitia mnyororo wa thamani
Rasilimali Asilia – Madini, Misitu, Wanyama pori
Ruvuma ni hazina ya madini kama makaa ya mawe, dhahabu na madini mengine adimu. Pia ina misitu mikubwa ya asili inayoweza kutumika kwa viwanda vya mbao na karatasi.
Kwa upande wa utalii wa ikolojia na uwindaji wa kitalii, maeneo mengi yanatoa fursa kwa uwekezaji wa hifadhi na nyumba za wageni.
Miundombinu ya Barabara
Kwa mwekezaji yeyote, miundombinu ni kipimo cha utayari wa eneo. Ruvuma imeunganishwa kwa kiwango cha lami ndani ya mkoa na na mikoa jirani. Hii inamaanisha bidhaa zako zinaweza kufika sokoni kwa haraka – iwe ni Songea, Mbeya, Mtwara au hata Dar es Salaam.
Kwa Nini Ruvuma?
Kwa sababu ina ardhi. Ina mvua. Ina watu. Ina barabara. Ina madini. Ina bandari. Ina kila sababu ya mwekezaji kufanikiwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.