MKOA wa Ruvuma umepokea shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa 156 katika Shule za sekondari mkoani umo kwani lengo la Serikali ni kuondoa changamoto ya upungufu wa madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Wilaya ya Songea ambayo imepokea shilingi bilioni 1.9 za ujenzi wa vyumba 96 vya madarasa.
Kanali Laban Thomas amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa katika Halmshauri ya wilaya ya songea na Madaba wakati alipofanya ziara katika Halmshauri hizo kwani ujenzi wa madarasa mengi yapo katika hatua ya mwisho ya utekelezwaji pia ujenzi wa madarasa hayo unatakiwa kumalika ifikapo Novemba 30,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.