• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma una hazina ya makaa ya mawe tani milioni 227

Imewekwa kuanzia tarehe: August 19th, 2020

Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Jumanne Mohamed Nkana anasema taarifa za tafiti za awali za makaa ya mawe katika maeneo ya Mbalawala Mbinga ni tani milioni 99.5, Mbuyula Mbinga tani milioni 15.1 na  Muhukuru Songea tani milioni 27.

Kwa mujibu wa Nkana tafiti katika eneo la Njuga  wilaya ya Songea tani milioni 23, Mbambabay katika kijiji cha Malini kata ya Mtipwili tani milioni 29, kijiji cha Liweta Kata ya Mbaha Nyasa tani milioni 34 na kwamba ubora wa makaa ya mawe yanayopatikana kwenye maeneo hayo yana wastani wa Calorific Value (CV)5,000 hadi 7,000.

Hata hivyo Afisa Madini Mkazi huyo wa Mkoa wa Ruvuma anasema uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe unafanyika katika maeneo ya Mbalawala,Mbuyula, Mbambabay, Muhukulu na Liweta.

Anawataja wateja wakubwa wa makaa ya mawe   yanayochimbwa katika maeneo hayo kwa sasa kuwa wapo ndani ya nchi na katika nchi jirani za Rwanda, Kenya na Uganda.

“Makaa ya mawe yanayozalishwa na kuuzwa kwenye masoko hayo ni kiasi cha wastani wa tani 55,000 kwa mwezi ambapo kati ya kiwango hicho asilimia 70 yanauzwa ndani ya nchi’’,anasema Nkana.

 Anaitaja hazina ya makaa ya mawe iliyopo kwenye maeneo hayo yote inakadiriwa kuwa  ni ziadi ya Tani milioni 227.6 ambapo uzalishaji unaofanyika kwa sasa ni wa wastani wa tani 55,000 na kwamba Inakadiriwa makaa hayo yatachimbwa kwa  miaka zaidi ya 300.

 Mataifa mengine yaliyoonesha nia ya kununua makaa ya mawe ya mkoa wa Ruvuma ni  India na China. Licha ya makaa ya mawe ya Ngaka  na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kuuzwa na kutumika viwandani ni muhimu kutumia makaa ya mawe kuzalishia umeme.

Mhandisi Nkana anabainisha kuwa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe gharama zake ni nafuu kwa wananchi na pia umeme huo utachochea ukuaji wa viwanda nchini hasa katika awamu ya tano ambayo inasisitiza serikali ya viwanda.

Utafiti umebaini kuwa umeme unaotokana na madini ya makaa ya mawe ndio unaotegemewa zaidi na mataifa mengi yaliyoendelea duniani.Takwimu zinaonesha kuwa makaa ya mawe yanachangia asilimia 41 ya umeme unaozalishwa duniani,umeme wa maji asilimia 16,umeme wa gesi asilia asilimia 20, nyukilia asilimia 15 na  umeme wa mafuta kwa kutumia jenereta ni asilimia sita tu.

Miongoni mwa mataifa yaliyoendelea kiuchumi  duniani ni yale ambayo yanatumia umeme wa makaa ya mawe.Mataifa hayo ni Afrika Kusini inayotumia asilimia 93 ya umeme wa makaa ya mawe,Poland asilimia 92 na China asilimia 79.Nchi nyingine ni Australia asilimia 77, Kazakhstan asilimia 70, India asilimia 69, Israel asilimia 63, Jamhuri ya Czech asilimia 60, Morocco asilimia 55,Ugiriki asilimia 52,Marekani asilimia 49 na Ujerumani asilimia 46.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.