MKOA wa Ruvuma una jumla ya hekta 197,108.2 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambapo hadi sasa ni hekta 7,388.3 ndizo zimeendelezwa sawa na asilimia 3.7
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Mkoa pia una skimu 102 za umwgiliaji na kwamba kati ya hizo skimu 42 zimeboreshwa,skimu 23 zinafanya kazi na skimu 19 hazifanyi kazi.
Hata hivyo amesema Tume ya Taifa ya umwagiliaji mkoani Ruvuma imefanikiwa kusajili skimu 42 katika kipindi cha mwaka 2020/2021 na kwamba katika kipindi cha mwaka 2022/2023 Tume hiyo imejipanga kukamilisha zoezi la usajili wa skimu 60 zilizobaki.
“Katika mwaka 2022/2023 skimu ya umwagiliaji Muhukuru wilayani Songea imepewa zaidi ya shilingi milioni 915 ili kutekeleza mradi huo ambao umepangiwa kufanyika kwa miezi 12’’,alisema.
Akizungumzia kilimo cha Pamoja,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema Mkoa umeanisha maeneo ya uwekezaji katika kilimo cha Pamoja ambapo jumla ya hekta 25,171.91 ambazo zimetambuliwa katika Halmashauri zote na kwamba maeneo hayo yatatumika kwa kilimo cha Pamoja.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.