Mkoa wa Ruvuma umeadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na maeneo mengine katika manispaa ya Songea ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika jijini Dodoma.
Akizungumza katika zoezi hilo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Jumanne Mwankhoo amewahimiza wananchi kuendelea kuwakumbuka mashujaa kwa kufanya usafi katika maeneo yote ya umma.
“Wito wangu kwa wanaruvuma wezangu nawaomba tuendelee kuwakumbuka na kuwaenzi Wazee wetu ambao wametoa uhai wao kwa ajili yetu na kupigania Nchi yetu ya Tanzania kwahiyo tuendelee kwakumbuka kwa kufanya usafi katika maeno ya Umma na maeneo yetu tuanayoishi” amesema Mwankhoo
Naye mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Dr. Louis Chomboko amesema zoezi la kufanya usafi ni endelevu na la umuhimu kwani mtu ni Afya hivyo wananchi waendelee kufanya usafi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kwani lazima tujue kwamba kesho yetu inajengwa na afya bora.
Maadhimisho haya ufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25, Julai.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.