• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma wachangia asilimia 3.8 ya Pato la Taifa

Imewekwa kuanzia tarehe: December 31st, 2022

MKOA WA RUVUMA WACHANGIA ASILIMIA 3.8 YA PATO LA TAIFA

UCHUMI wa Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuimarika kwa kuchangia asilimia 3.8 ya pato la Taifa ukiwa juu ya mikoa mingine ya Kanda ya Kusini Mashariki.

Kwa mujibu wa Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,uchumi wa Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuimarika ambapo Pato la Taifa (GDP) kwa bei za mwaka husika,pato la Mkoa liliendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 3.147 mwaka 2014 hadi kufikia shilingi bilioni 6.106 mwaka 2021.

Mchumi Mkuu kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Kanda ya Mtwara Peter Stanlaus akizungumzia hali ya uchumi wa Mkoa wa Ruvuma kwenye kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa wa Ruvuma(RCC) amelitaja wastani la pato kwa mtu (GDP per capital) katika Mkoa limeendelea kuongezeka na kuwa juu ya wastani wa pato la mtu kitaifa.

“Wastani wa pato kwa mtu kwa mwaka katika Mkoa wa Ruvuma liliongezeka kutoka shilingi 2,184,532 mwaka 2014 hadi kufikia shilingi  3,602,162 mwaka 2021 ikilinganishwa na wastani wa pato kwa mtu kitaifa la shilingi 2,798,244 kwa mwaka’’,alisema.

Hata hivyo Mchumi Mkuu huyo wa BOT amesema hali ya mfumko wa bei katika Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha mwaka 2021/2022 ulibakia kwenye wastani wa asilimia 3.2 kutokana na kuimarika kwa ugavi wa chakula na kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula.

Akizungumzia  Mkoa wa Ruvuma ulivyochangia uchumi kupitia sekta ya madini,Mchumi Mkuu huyo wa BOT amesema sekta ya madini imeendelea kuimarika katika Kanda ya Kusini Mashariki ambapo kwa mwaka 2021/2022 ilichangia shilingi bilioni 728.9.

Hata hivyo ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa katika sekta ya madini kwenye Kanda hiyo,ulichangia asilimia 69.9 ya thamani ya mapato yote ambapo uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe kutoka Ruvuma pekee umechangia asilimia 96.4 ya thamani ya madini yote kanda ya Kusini Mashariki.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo ya BOT,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewapongeza wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma hasa kwenye sekta za kilimo na madini  walivyoshiriki kikamilifu kuimarisha uchumi wa Mkoa.

“Kabla ya ripoti hii nilidhani naongoza Mkoa masikini,kumbe Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa tajiri kwa sababu pato la mtu lipo juu ya wastani wa pato la mtu kitaifa’’.alisisitiza RC Thomas.

Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuwa kapu la chakula la Taifa kwa kuongoza mfululizo kitaifa kwa miaka minne katika uzalishaji wa chakula nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Desemba 31,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.