Mkoa wa Ruvuma wafurahishwa na kasi ya utelezwaji wa miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Katika miaka yake miwili tangu aingie madarakani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameeleza kuwa Mkoa wa Ruvuma haujachwa nyuma katika kupewa miradi mikubwa ya maendeleo ambapo tangu Rais samia aingie madarakani ametoa fedha kila sekta kwa lengo la tutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi
“Namshukuru Rais Samia kwa kuhakikisha Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanakuwa sehemu bora ya kuboreshewa huduma mbalimbali za kimaendeleo sote ni mashahidi tumoena akitoa fedha katika sekta ya Afya, Barabara, Maji, Elimu na Kilimo.”
Pia Kanali Thomas amesema Mkoa wa Ruvuma ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwani kwa msimu wa 22/23 Mkoa umepokea tani 65,000 za mbolea kati ya tani 67,000 zinazotarajiwa
Hata hivyo ameeleza kwa upande wa sekta ya maji Mkoa umepokea pesa nyingi za ujenzi wa miradi ya maji ambapo kwa msimu wa 22/23 Mkoa unaendelea kutekeleza miradi 33 yenye thamani ya shilingi bilioni 51.2. amesema miradi hiyo ikikamlika itakuwa unahudumia wananchi wapatao 264,000 na Vijiji 81.
Aidha, katika miaka miliwi ya Rais samia Serikali imetoa bilioni 3.2 kujenga vyumba vya Madarasa 156 katika Shule za sekondari mkoani Ruvuma vili vile na sekta ya Afya ameweza kuongeza mradi wa vituo vya Afya katika Halmashauri zote na baadhi yake vimeshanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.