• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma washika nafasi nzuri ukusanyaji mapato kitaifa

Imewekwa kuanzia tarehe: January 19th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme amewapongeza Wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kusimamia ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo Halmashauri zote nane zimevuka  asilimia 80 na kufanya Mkoa kuwa katika nafasi nzuri Kitaifa.

Mndeme pia ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa wa Ruvuma kwa kufanya kazi nzuri ya kukusanya Mapato ya ndani  ya Mkoa  katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na kuweza kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 15 sawa na asilimia 94.

“Naipongeza Halmashauri ya Tunduru  kwa kukusanya Mapato ya Ndani kwa asilimia 121.87,pia naipongeza Halamashauri ya Manispaa ya Songea tangu  imeanza kutumia stendi kuu ya Shule ya Tanga Januari1,2021  imeongeza mapato kutoka shilingi 200,000 mpaka  970,000 kwa  siku”,alisema.

Mndeme amesema Mkoa unatarajia kuimarika kiuchumi kwa kuongezeka kwa mapato yatokanayo na kodi pamoja na ushuru kwasababu Barabara ya Ushoroba wa  Mtwara imefunguka na kupelekea kutoa fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi.

Hata hivyo amesema biashara ambazo zinapatikana maeneo mengine Nchi Jirani za Malawi na Msumbiji yanaunganishwa kwa kupitia usafiri wa Ndege kupitia Uwanja wa ndege wa Songea na barabara ya lami ya Mtwara corridor.

Amesema Meli katika Ziwa Nyasa zimeanza kazi za Usafirishaji baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Meli ya abiria ya MV Mbeya  II Januari 5,2021 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Kassim Majaliwa ambayo inabeba abiria  300 na Mizigo tani 200.

Hata hivyo Mndeme amewaagiza Wakurugenzi kusimamia Mapato yatokanayo na Kodi pamoja na Ushuru amesema fedha hizo hutumika katika kujenga miradi ya maendeleo ikiwemo vituo vya Afya,Barabara,Ununuzi wa Ndege,Ujenzi wa Reli na  huduma nyingine za kijamii.

Ameziagiza Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma kubuni na kupanua wigo wa mapato kwa kuhimiza watu kudai Risiti na wafanyabiashara  kutoa risiti kila wanapouza  bidhaa mbalimbali.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Januari 19,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.