MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amedhamiria kuona huduma ya maji safi na salama inaendelea kuimarishwa na kuwafikia wakazi asilimia 85 wa vijijini na mjini 95 .
Ibuge amesema kuwa wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini wanaopata huduma ya maji safi na salama wanakadiriwa kuwa 833,361 ni sawa na asilimia 62.
Mkoa kupitia ofisi za RUWASA umeingia mkataba na local mafundi kwaajili ya kutekeleza miradi hiyo kwa kutumia Force Akaunti miradi inayoendelea na ukarabati.
Aidha, miradi mipya 20 ambayo inatarajia kuhudumia vijiji 52 ipo kwenye hatua za ununuzi wa wakandarasi kupitia mfumo wa ununuzi wa serikali TANePs.
Ibuge ameeleza mpango wa utekelezaji miradi ya Maji Vijijini lipa kwa matokeo awamu ya tatu ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kiasi cha shilingi Zaidi ya bilioni 1 kimepokelewa kwaajili ya ukarabati na upanuzi wa miradi 29.
Hata hivyo amesema utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2021/2022 Mkoa wa Ruvuma kupitia ofisi ya Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mpaka octoba 2021 imepokea Fedha kiasi cha Zaidi ya shilingi bilioni sita kwaajili ya kukamilisha miradi 21 inayoendelea.
“Mpango wa wa Bajeti ya mwaka 2021/2022 Mkoa kupitia ofisi ya RUWASA Mkoa umetengewa jumla ya Zaidi ya shilingi bilioni 13”.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Januari,31 2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.