Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Nyasa ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Bw.Khalid Khalif akipiga kura ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa katika kituo cha Kilosa Kati,Kata ya Kilosa wilayani Nyasa
Wakati huo huo Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Nyasa Bw. Khalid Khalif amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kukamilisha zoezi la upigaji kura kwa amani na utulivu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake amesema zoezi la upigaji kura limekamilika salama kinachoendelea kwa sasa ni kuhesabu kura na kutoa matokeo .
Bw Khalif amefafanua kuwa zoezi la kupiga kura kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa limeanza saa Mbili kamili asubuhi Tarehe 27/11/2024na kukamilika saa 10 jioni, na kwa sasa Zoezi linaloendelea ni kuhesabu kura.
“Wananchi wameendesha zoezi hili kwa amani na utulivu na kila eneo liko shwari hivyo nichukue fursa hii kuwapongeza sana wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuendesha shughUli hii kwa amani na Utulivu”
Kwa upande wao wananchi waliofanya mahojiano wakiwemo mawakala wa Chama cha CCM , Chadema Act wazalendo na wananchi wa kawaida wamesema wameridhishwa na mwenendo mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na wanachosubiri kwa sasa ni matokeo ambayo yatawapa viongozi bora ambao wamewachagua.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.