• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa azindua Bodi ya PAROLE Mkoa wa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: March 3rd, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge ambae amewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololet Mgema amezindua Bodi ya PAROLE Mkoani Ruvuma.

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.

Akizungumza kabla ya Uzinduzi huo amempongeza Mwenyekiti wa Bodi hiyo pamoja na wajumbe wote kwa kuteuliwa katika nafasi hii ya muhimu.

Hata hivyo Mgema amesema kuteuliwa kwao kuwa wajumbe wa Bodi kumetokana na kukidhi vigezo pamoja na uwezo wao ambao utasaidia Bodi ya Mkoa wa Ruvuma kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kwa ufanisi mkubwa.

‘’Ndugu wajumbe majukumu ya Bodi ya PAROLE kama ilivoainishwa katika sheria  ni kama ifuatavyo kupitia na kujadili majalada ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika na mpango, pia kutoa mapendekezo kwa wafungwa waliokidhi vigezo vya kunufaika na mpango pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya majalada ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika na mpango wa PAROLE’’ amesema Mgema.

Kwa upande wake Katibu wa Bodi ya PAROLE ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma  Kamishna Msaidizi wa Magereza Willington Willbard amewataja wajumbe wa Bodi ya PAROLE jumla wapo 11  kati yao wajumbe watano wameteuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na wajumbe  sita wameainishwa na Sheria ya PAROLE ya iliyopitishwa na Bunge ya 1994.

Naye Mjumbe wa Bodi ya PAROLE akizungumza kwa niaba ya wajumbe wake Vestina Nguruse ametoa shukurani kwa Mgeni rasmi kwa maneno  mazuri, maelekezo ya miongozo na ufafanuzi wa mambo ya msingi pia wamehaidi kutekeleza jukumu hili kwa uaminifu na uzalendo.

PAROLE ni utaratibu wa wafungwa kutumikia kifungo nje ya gereza kabla ya kumaliza kutumikia vifungo vyao baada ya kukidhi sifa na vigezo vilivoainishwa katika Sheria ya PAROLE.

Imeandaliwa na Bahati Nyoni

Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Machi 3 2022.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.