MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge amewataka skauti wajitambulishe kwa nafasi zao ili kujitofautisha na vijana wengine wa mitaani.
Ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Songea Club mjini Songea.
RC Ibuge amesema Skauti inalenga kuwapa malezi vijana yatakayowafanya wawe raia wema wenye uzalendo wa kuipenda Nchi yao.
Aidha, amewataka Skauti kutumia Rasilimali zilizowazunguka kama vile kujihusisha na kilimo au ufugaji nyuki ili waweze kujiwezesha.
"Skauti ninachoipendea maandalizi yako yanakuandaa uitumikie Nchi yako kwa jasho lakini ata kwa damu ikibidi", amesema RC Ibuge.
RC Ibuge amesema anatambua umuhimu wa Skauti kwenye ulinzi wa Nchi, kujitambua na mchango wake kwenye jamii inayomlea, kulinda uhuru na hadhi ya Taifa pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa ya mambo mabaya yanapoonekana kufanyika.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Skauti Mkoa wa Ruvuma Mourice Lugongo amesema chama cha Skauti kina mahusiano mazuri na Serikali, viongozi wake pamoja na jamii kiujumla, pia imefanikiwa kujiunga na Taasisi mbalimbali kama Taasisi ya kupambana na rushwa Takukuru.
Skauti ni chama kinachowalea vijana kwaajili ya kupambana na maisha ya hapo baadae.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.