MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa amewashauri wananchi wilayani Tunduru kupata taarifa sahihi kutoka kwa watalaam wa afya kuhusu umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO 19 badala ya kutumia taarifa ambazo sio sahihi ambazo zinatolewa katika mitandao mbalimbali.Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkowela Kata ya Namakambale amesisitiza ni muhimu kutumia taarifa za wataalam wa afya ili wasiendelee kupotoshwa kwa sababu wataalam wamethibitisha kitaalam kuwa chanjo hiyo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amechanjwa na yeye mwenyewe kama Mkuu wa Mkoa amechanjwa.
Tazama habari kwa kina hapa https://www.youtube.com/watch?v=YBk2jo9vwWE&t=50s
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.