Ahimiza wananchi kutunza mazingira
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewaomba wanachi kulinda mazingira na vyanzo vya maji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Mkuu wa Mkoa ametoa rai mara baa da ya kutembelea chanzo cha Mto Ruvuma kilichopo katika milima ya Matogoro mjini Songea.
Amesema kulinda vyanzo vya maji kutapunguza uhalibifu wa mazingira na amewataka viongozi wezake kuwahimiza wananchi walinde misitu kwa uifadhi wa mazingira ya sasa na ya baadae
“Tujisike fahari kwa kuwa na vyanzo hivi na tuvuenzi tena nitoe wito kama tulivyo sikia changamoto za moto niwajibu wetu sisi wananchi kilinda mazingira yetu na vitu vyetu vya asili”
RC Thomas ameyasema hayo alipotembelea chanzo cha mto Ruvuma kilichopo katika mlima wa matogora ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye siku ya uzinduzi wa Makala maalumu ya utalii mkoa wa ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.