• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma atoa maagizo 20 kwa Halmashauri mbili zilizopata hati zenye mashaka

Imewekwa kuanzia tarehe: June 21st, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametoa maagizo 20 kwa Halmashauri mbili zilizopata hati zenye mashaka ili ziweze kubadilika na kurejea kwenye hati safi.

Kanali Thomas ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti katika Halmashauri za Mbinga Mji na Nyasa ambazo zimepata hati zenye mashaka wakati anazungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ni Pamoja na kufunga hoja zote zilizosalia,kuzuia kujirudia kwa hoja,wakuu wa Idara kushiriki kuandaa kikamilifu majibu ya hoja na Halmashauri kuchukua hatua za kinidhamu mapema kwa watumishi wanaozalisha hoja.

“Hakikisheni taarifa za hesabu za mwisho za  mwaka zinaandaliwa kwa kuzingatia matakwa ya viwango vya kihasibu vya kimataifa katika sekta ya umma na Afisa Masuuli uhakikishe unashiriki mwenyewe katika vikao vya wakaguzi’’,alisisitiza.

Maagizo mengine ni  kudhibiti upotevu wa mapato katika Halmashauri,marufuku kutumia fedha mbichi,fedha zote zinazokusanywa lazima ziingizwe kwenye mfumo wa mapato na kuwasilishwa  benki,kuzingatia sheria za manunuzi na Halmashauri kuendelea kulipa madeni mbalimbali ya wazabuni.

Mkuu wa Mkoa pia ameagiza  kufanyika mara kwa mara vikao vya Kamati ya ukaguzi wa Hesabu katika Halmashauri,kufuatilia wadaiwa sugu wa mapato ya Halmashauri,kusimamia kikamilifu mfuko wa Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa,kutoa elimu kwa wanufaika wa asilimia kumi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa amesikitishwa na Halmashauri hizo kupata hati zenye mashaka katika matokeo ya ukaguzi ambao ulifanywa na CAG katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2022.

Hata hivyo amesema licha ya kupata hati zenye mashaka,mwenendo wa kushughulikia Hoja na Mapendekezo ya CAG katika Halmashauri hizo  bado hauridhishi.

Ameuagiza Uongozi wa Halmashauri hizo kuhakikisha kuwa wanakamilisha utekelezaji wa kujibu hoja na mapendekezo yote ya CAG kabla ya Septemba 30,2023.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakurugenzi wa Halmashauri za Mji wa Mbinga na Halmashauri ya Nyasa wameahidi kutekeleza kikamlifu maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha Halmashauri hizo katika ukaguzi ujao wa CAG wanarejea kupata hati safi.

Mkoa wa Ruvuma una Halmashauri nane kati ya hizo Halmashauri sita zimepata hati safi na halmashauri mbili zimepata hati zenye mashaka katika matokeo ya ukaguzi wa CAG uliofanywa katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2022.

Mwisho.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.