Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amezitaka kamati za kudhibiti na kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoani Ruvuma kuhakikisha wanatokemeza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Mndeme ametoa maagizo hayo wakati amefanya ziara ya siku moja wilayani Namtumbo a mbapo amesisitiza waendelee kutoa elimu ili kuweza kupambana na virusi vya ukimwi na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.
“Kamati ya UKIMWI ijitahidi kutoa elimu kwa watoto,vijana na watu wazima huko majumbani kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi.”Amesema Mndeme.
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI wilaya ya Namtumbo Fidelis Mkini,amesema katika kipindi cha mwaka 2019 jumla ya watu 45,076 walipimwa kati yao waliogundulika kuwa na maambukizi ni 587 na kwamba maambukizi yamepungua kutoka asilimia mbili ya mwaka 2018 mpaka asilimia moja kwa mwaka 2020.
Muguzi Mkunga katika kituo cha afya Namtumbo Evarister Ngailo amesema wateja wakifika katika kituo hicho wanapimwa wakikutwa na maambukizi ya vvu wanawaanzishia huduma endelevu ambazo ni dawa za ARV na kumfatilia mteja ndani ya siku 14.
Godwin Rutta Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Namtumbo,amesema katika kituo kipya wameanza kutoa huduma za upasuaji ambapo hadi sasa wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji wagojwa 125 ambao wote wamefanyiwa upasuaji bila kupata changamoto zozote.
Imeandikwa na Farida Musa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.