MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameuagiza uongozi wa SUMA JKT kuongeza wafanyakazi ili kukamilisha ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambapo hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 50.
Kanali Thomas ametoa agizo hilo baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambalo serikali imetoia shilingi bilioni tatu kutekeleza mradi huo ambapo hadi sasa zimetumika zaidi ya shilingi bilioni mbili kutekeleza mradi huo ambao unatarajia kutumia shilingi bilioni tano hadi kukamilika kwake.
Amesema Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anajitahidi kutoa mabilioni ya fedha za kutekeleza miradi mbalimbali nchini,hata hivyo usimamizi wa miradi usiokuwa na tija unachelewesha baadhi ya miradi kuchelewa hivyo amewaagiza madiwani katika Halmashauri zote kusimamia kikamilifu miradi yote ya maendeleo a,mbayo haijakamilika kwa muda mrefu ili iweze kukamilika kwa tija na ubora unaolingana na thamani ya fedha..
Akitoa taarifa ya ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangasongo alisema ujenzi wa mradi huo unatarajia kukamilika kwa asilimia 100 Machi mwakani ambap ameitaja changamoto kubwa inayochelewesha mradi huo kukamilika ni Mkandarasi wa ujenzi kuwa na idadi ndogo ya wafanyakazi wanaotekeleza mradi huo hali ambayo imechelewesha mradi kukamilika ndani ya mkataba. hivyo ametoa wito kwa SUMA JKT kuongeza idadi ya watumishi ili kukamilisha ujenzi wa jengo hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.