Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amezindua WILOLESI FOUNDATION MARATHON 2024 Katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea.
Katika uzinduzi huo ulioshirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile.
Mkurugenzi wa WILOLESI FOUNDATION Dr Gofrey Mdede amelitaja lengo la Foundation hiyo kuwa ni kuchangia vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea (HOMSO) ili kuokoa maisha ya watoto wachanga wanaozaliwa njiti katika hospitali hiyo.
Ameongeza kuwa pia Foundation hiyo inasimamia na kuratibu Marathon 2024 ambazo zinatarajia kufanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea kuanzia Januari 12,2024
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.