MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la Biashara na Uwekezaji la Mkoa wa Ruvuma.
Kongamano hilo linatarajia kuwa na washiriki 220 kutoka mkoani Ruvuma na kufanyika Septemba 15,2023 kwenye ukumbi wa Manispaa mjini Songea.
Wadau wa biashara na uwekezaji mkoani Ruvuma watatangaza fursa za kiuchumi zilizopo mkoani Ruvuma katika sekta za madini,kilimo,uchumi wa buluu ikijumuisha ziwa Nyasa na Mto Ruvuma,miundombinu ya usafirishaji,umeme na maji.
Kongamano hilo litakuwa mbashara kwa saa tatu kuanzia saa 3;00 asubuhi hadi saa sita mchana kupitia WASAFI MEDIA,pia vyombo mbalimbali vya Habari vimealikwa kwenye kongamano hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.