Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mheshimiwa .Filberto Sanga, akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama na wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa amefanya Ziara ya kikazi ya kutembelea, na kukagua miradi ya Maendeleo katika kata za Kilosa na Mbamba bay.
Miradi aliyotembelea ni mradi wa Ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya sekondari Limbo unaogharimu shilingi milioni 150 na mradi wa ukamilishaji wa bweni la wasichana katika sekondari ya Limbo ambao unagharimu shilingi milioni 40.
Miradi mingine, ni mradi Boost wa shule mpya ya msingi Kilosa wenye thamani ya shilingi milioni 370, ambao uko ngazi ya msingi, mradi wa ukamilishaji wa darasa Moja na Ofisi katika shule ya msingi Mbamba bay na mradi wa GPE LANES Ii unaogharimu shilingi 22,000,000, pamoja na mradi wa boost katika Shule ya msingi Nangombo, madarasa 2 mradi ambao unaogharimu TSH milioni 77.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Mheshimiwa Sanga amewataka mafundi kufanya kazi Kwa bidii na kuhakikisha kuwa wanakamilisha Kwa wakati Na ubora ifikapo Juni 30. 2023.
Aidha amewaagiza mafundi Ujenzi wote kuhakikisha wanajenga Kwa kufuata vipimo vilivyotolewa na Serikali na kuzitaka kamati zote kuhakikisha zinatekeleza majukumu yake Kwa kufuata Sheria kanuni na taratibu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.