MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Wilman Kapenjama Ndile amewataka Viongozi wa Kata na Vijiji kuendelea kusisitiza wananchi kupanda miti katika maeneo ya Shule, Hospitali na katika taasisi za serikali kwa lengo la kutunza mazingira.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake yenye lengo la kuongea na wananchi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kukagua miradi ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Songea
Akizungumza katika shule ya msingi Mbolongo amewataka walimu waendeelee kusisitiza wazazi katika suala zima la kuchangia chakula ili wanafunzi waweze kupata chakula shuleni.
Aidha, amewapongeza uongozi wa shule ya msingi Mbolongo kwa mpangilio mzuri wa ratiba na mpango kazi hivyo amewaahidi kuwatengenezea kabati (shelf) kwaajili ya kuhifadhia vitabu.
Pia DC Ndile ametembelea shule ya msingi Selekano ambapo amewataka Viongozi wa Kata na Kijiji Pamoja na wataalamu kusimamia vyema fedha zinazokuja kwaajili ya kutekeleza miradi ili iweze kukamilika kwa viwango vinavyokubaliwa na Serikali kwani inawapa matumaini Viongozi wanaoleta fedha na wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.