Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanai ya Kijiji cha Mbangamawe Kata ya Gumbiro katika Halmashauri ya Madaba ambayo imejengwa kwa Shilingi Milioni 110 .
Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo Oddo Mapunda amesema katika ujenzi huo walipokea fedha za ujenzi kutoka Serikali kuu awamu ya kwanza Milioni 50, awamu ya pili Milioni 50 na nguvu za wananchi Milioni 10.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amesema bajeti ya mwaka mpya wa Fedha 2023/2024 itaboresha huduma katika Zahanati hiyo kwa kuongeza huduma ya vipimo na Dawa hali ambayo itasababisha zahanati hiyo kutoa huduma ya kiwango cha kituo cha Afya.
Zahanati hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.