Shule ya sekondari ya Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imenufaika na fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya baada ya kujenga madarasa 11 yanayogharimu shilingi milioni 220.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 1.5 kujenga madarasa 76 katika shule za sekondari katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Menejimenti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imekagua mradi wa madarasa hayo ambayo yanatakiwa kuchukuwa wanafunzi kuanzia Januari 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.