Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme, ameitaka jamii kuacha ukatili wa kijinsia, na wahamasike kuongeza fursa za Kiuchumi kwa Wanawake kwa kuwajengea uwezo wa kitaalam, kibiashara, na mbinu za kupata mtaji na masoko.
Aliyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wanawake, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kimkoa yaliyofanyika katika Viwanja vya Polisi ,Mjini Mbamba-bay Wilayani hapa.
Mndeme aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, alifafanua kuwa, jamii inatakiwa kuacha mara moja Ukatili wa kijinsia, na badala yake wahamasike kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake,kwa kuwajengea uwezo wa kitaalam, kibiashara, na mbinu za kupata mtaji wa masoko ili waondokane na utegemezi.
Aliongeza kuwa, Serikali na wadau kwa ngazi zote, haina budi kuendelea kuweka vipaumbele vya kuwainua Wanawake Vijijini, ili waweze kuwa Wajasiliamali wenye bidhaa bora na kuwatafutia masoko ya Kimataifa kwa lengo la kuitangaza nchi yetu, na kuinua uchumi wa Taifa letu.
“jamii haina budi kuongeza fursa za Kiuchumi kwa Wanawake ili kuwajengea uwezo wa kitaalam, kibiashara, mbinu za kupata mtaji na masoko. Serikali na wadau na ngazi zote kuendendelea kuweka vipaumbele vya kuwainua Wanawake Vijijini waweze kuwa Wajasiliamali wenye bidhaa bora na kuwatafutia masoko ya Kimataifa kwa lengo la kuitangaza nchi yetu lakini vilevile kuinua uchumi wa Taifa letu.
Naye mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Bi Zawadi Nyoni , akitoa maelezo ya idara yake alisema , amewahamasisha wanawake wengi kujiunga na kuanzisha vikundi vya wanawake ili kuvipatia mikopo mbalimbali, na hadi Desemba 2019 jumla ya vikundi vya wanawake 389 vimeundwa na kukopeshwa tsh 509,174,487.00 ikiwa ni fedha za asilimia kumi za mapato ya ndani za Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma.
Bi Nyoni aliongeza kuwa idara yake inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii, uhaba wa vitendea kazi ikiwemo usafiri, kutopewa fedha za asilimia kumi kwa wakati na hata zikipatikana hazikidhi mahitaji ya waombaji wa mikopo.
Maadhimisho hayo yameambatana na shughuli mbalimbali zilizofanyika Wilayani hapa, ikiwa ni pamoja na Kongamano la Wanawake wajasiliamali ambapo walipewa elimu ya ujasiliamali na elimu ya kuzifahamu haki na Sheria za ndoa na Mirathi, pamoja na kutembelea na kutoa misaada mbalimbali katika wodi ya wazazi (Maternity) katika kituo cha afya cha Mbamba-bay Wilayani Nyasa.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni sabuni ya unga mifuko mitatu,buti pea tisa, sabuni za mche katoni tatu, mpira ya kutandika kitandani meta nane, brash za kufanyia usafi 6, Ndoo za taka 06, ndoo za kudekia 04.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.