SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli inatekeleza mradi mkubwa wa maji katika Mji wa Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.Meneja wa RUWASA wilaya ya Songea Mathias Pangras amesema mradi umekamilika kwa asilimia 75.
Amesema mradi umejengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza walijenga chanzo na tank la lita laki mbili,na awamu ya pili wameongeza kujenga tank mbili na kazi ya usambazaji wa maji kutoka kwenye tank kwenda kwa wananchi.
Mathias amezitaja gharama ya ujenzi ni zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni sabini na tisa, na mradi ukikamilika utamaliza tatizo la maji katika wilaya ya Madaba.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya songea Pololeti Mgema ametoa maagizo kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kutoa elimu kwa wananchi wa Madaba kuhusu umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.
Mgema ametoa maagizo hayo hivi karibuni wakati alipotembelea na kukagua chanzo cha maji cha Mgombesi kilichopo kilomita tano kutoka barabara kuu ya Songea - Njombe.
Mgema amesema wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kiuchumi karibu na vyanzo ya maji wapewe elimu kuhusu umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na athari zake kwa viumbe hai.
Mgema amesisitiza kwakusema wananchi wote wanaofanya shuguli za kiuchumi karibu na vyanzo vya maji ni marufuku kufanya kazi hizo kwalengo la kukabiliana na changamoto za ukosefu wa maji.
“ Maagizo yangu vyanzo vya maji vilindwe”,amesema Mgema.
Amesisitiza wataalam wa RUWASA kuongeza juhudi za kukamilisha ujenzi wa mradi huo ili uweze kutoa huduma kwa wananchi kama Serikali inavyopambana kuondoa tatizo la maji katika jamii.
Mgema amesema zaidi ya wakazi 30,000 wa vijiji vya kipingu,kifagulo,Mtepa na Lituta ndio wanufaika wakuu wa huduma hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Kijiji cha Lituta na kipingu Esta Mlelwa na Godfrey Ngatunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha kipingu anakili kuwepo kwa tatizo la maji katika vijij hivyo lakini kwa sasa wanatoa shukrani kwa serikali kwa kuwaletea huduma ya maji
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.