• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MRADI WA BOOST kujenga madarasa 12,000 na shule salama 6,000

Imewekwa kuanzia tarehe: December 17th, 2022

WATAALAM zaidi ya 280 kutoka ngazi za Halmashauri na mikoa ya Ruvuma,Njombe na Iringa  wamepata mafunzo elekezi ya timu za utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) unaogharimu sh.trilioni 1.15 wenye lengo la kujenga madarasa 12,000 na shule salama 6,000 katika nchi nzima.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI yamefanyika kwa siku mbili katika shule ya sekondari Lugalo Manispaa ya Iringa.

Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo,Mratibu wa Mafunzo kutoka Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Yusuph Singo  amesema TAMISEMI imeandaa mafunzo hayo katika Kanda tisa kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wa timu hizo kuhusu usimamizi wa mradi wa BOOST.

Amezitaja timu hizo kuwa zinaundwa na wajumbe 12 kutoka ngazi ya Halmashauri ambao ni Afisa Elimu Msingi,Afisa Maendeleo ya Jamii,Mhandisi,Mwalimu Mkuu,Afisa Manunuzi,Mthibiti Ubora wa Shule, Afisa Ustawi wa Jamii,Afisa Elimu Kata,Afisa Mipango,Afisa Habari na Mratibu wa Mradi.

Amesema katika ngazi ya Mkoa timu inaundwa na wajumbe wanane ambao ni Afisa Elimu Mkoa,Mratibu wa Mradi wa BOOST,Mhandisi,Afisa Habari,Afisa Maendeleo ya Jamii,Afisa Ustawi wa Jamii,Afisa Mipango na Mdhibiti Ubora wa Shule Kanda.

“Mheshimiwa Rais ametafuta fedha kiasi cha shilingi Trilioni 1.15  kwa ajili ya uboreshaji mkubwa wa elimu kupitia Mradi wa kuimarisha ujifunzaji shule za msingi na awali, utekelezaji wa mradi huu ni wa miaka mitano utaboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufundishaji’’,alisisitiza Singo.Baadhi ya washiriki wa  mafunzo elekezi ya Timu za utekelezaji wa mradi wa BOOST kutoka mikoa ya Ruvuma,Iringa na Njombe wakiwa kwenye mafunzo katika shule ya sekondari Lugalo Manispaa ya Iringa

Amesema mradi utatekelezwa katika afua mbalimbali  ikiwemo kuboresha miundombinu ya shule za msingi kwa kuzingatia mahitaji hususan ujenzi wa madarasa, uimarishaji wa mpango wa shule salama, kuimarisha uwiano wa uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, kuboresha vifaa na njia za ufundishaji elimu ya awali, pamoja na kuimarisha na kuendeleza mpango wa mafunzo ya walimu kazini.

Mratibu huyo wa Mafunzo wa TAMISEMI amesema katika kipindi cha miaka mitano madarasa 12,000 yatajengwa nchi nzima katika shule za msingi kupitia mradi wa BOOST na kwamba kwa kila mwaka yanatarajiwa kujengwa madarasa 3,000 ambapo afua zote zitatekelezwa kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo(EP4R).

Hata hivyo amesema kupitia mradi wa BOOST shule za msingi 800 zinatarajiwa kuwekewa vifaa vya TEHAMA ili kuwawezesha walimu kujifunza utoaji wa elimu endelevu hivyo kuboresha elimu ya msingi.

 Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Shule Salama kitaifa Hilda Mgomapayo amesema kupitia mradi wa BOOST  shule salama 6,000 zinatarajiwa kujengwa katika nchi nzima katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mradi huu ambapo katika awamu ya kwanza zinatarajiwa kujengwa shule 1000.

Amesema shule salama zitawajengea uwezo wanafunzi kujiamini katika mfumo wa elimu,kuimarisha stadi za Maisha,mawasiliano na mahusiano hivyo Watoto kufikia malengo yao.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Lugalata Mwshemi akizungumzia afua ya kuongeza uandikishaji Watoto wa awali,amesema kupitia mradi wa BOOST inatarajiwa kuboresha, uandikisha wa wanafunzi elimu ya awali kwa kuongeza idadi ya wanafunzi katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji.

Amesema katika utekelezaji wa mwaka wa kwanza uandikishaji wa elimu ya awali 2021/2022 unatarajiwa kuwa ni asilimia 75,mwaka 2022/2023 asilimia 80.14,mwaka 2023/204 asilimia 81.76,mwaka 2024/2025 asilimia 83.38 na mwaka 2025/2026 kuwa asilimia 85.

Hata hivyo amesema lengo ni kuhamasisha jamii kuhusu uandikishaji wanafunzi wa awali wenye umri wa kati ya miaka mitatu hadi mitano na kuhakikisha wanafunzi wote waliondikishwa wanakamilisha mafunzo kwa mwaka mmoja.

Takwimu zinaonesha kuwa hapa nchini kuna shule za msingi zaidi ya 17,000,hata hivyo kupitia mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) watoto zaidi ya milioni 12 wanatarajia kunufaika na mradi huo.

 

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma.

Desemba 17,2022

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.