MENEJA wa sikauti wa kike wa Lishe Tanzania David Mbamila amesema mradi wa lishe kwa watoto wa kike mkoani Ruvuma unatarajia kuanza hivi karibuni.
Mbamila amelitaja lengo la mradi huo ni kufanya mafunzo kwa walimu wa mkoa wa Ruvuma ili kutekeleza elimu ya lishe kwa watoto wa kike kuanzia miaka sita hadi 18.
Mbamila amesema mradi huo utaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Oktoba na Novemba 2020 kwa kutumia shule na walimu kwa lengo la kutoa elimu ya lishe kwa mtoto wa kike ambaye anakabiliwa na changamoto ya kupoteza damu nyingi wakati wa hedhi katika mzunguko wa kila mwezi.
Katibu wa Chama cha Maskauti wa Kike Taifa (Girl Guides association Tanzania) Bupe Minga ametoa mafunzo ya lishe bora kwa walimu wa shule za Sekondari na Msingi wa Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa sekondari ya Songea Girls,Minga amesema chama hicho cha maskauti wa kike Tanzania kimefungua matawi katika mikoa 23 ikiwemo Ruvuma.
Amesema kupitia mafunzo hayo kamati ya uongozi Taifa Inatarajia kutoa uhamasishaji kwa skauti wa kike kufahamu lishe bora kwa mtoto wa kike.
Amesema Mkoa wa Ruvuma ambao unaoongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini utavuma katika uelekeo wa sikauti kwa mtoto wa kike kupata chakula bora kupitia mfumo wa sikauti kwa mtoto wa kike
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Kisongo amewaagiza walimu hao kuhakikisha kuwa kila shule iwe na sikauti ya wasichana(Girl Guides) kwa sababu watoto wa kike ni lulu katika jamii.
“Watoto wa kike wamebeba moyo mkubwa kuleta ukombozi na amani dunia wakati wote na mpambanaji mkubwa ndio maana Serikali inamtumia hata usalama wa nchi unategemea girl Guides hawawezi kusaliti nchi”,alisisitiza.
Kisongo amesema Walimu wanayokazi ya kuhakikisha wanafunzi wanajitambua na kuhakikisha wanakuwa salama kiafya hata katika Lishe bora na kielimu kwa .sababu mtoto wa kike ni ukombozi na matokeo salama.
Kamishna wa masikauti wa kike mkoa wa Ruvuma Stella Sangu, amesema amefarijika katika elimu ya Lishe kwa mtoto wa kike ambapo amesisitiza kuwa ukimuelimisha mtoto wa kike umeelimisha jamii nzima.
Imeandaliwa na Aneth ndonde
Ofisi ya habari mkoa wa Ruvuma
17 August 2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.