• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MRADI wa maji Nangombo kunufaisha wananchi 13,323

Imewekwa kuanzia tarehe: June 2nd, 2024

MRADI wa maji Nangombo -Kilosa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma  unaotekelezwa kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni nne unatarajia kuwanufaisha wananchi wapatao 13,323 utakapokamilika.

Hayo yamesemwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya  Nyasa Mhandisi Masoud Samila wakati anatoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed .

Amesema mradi huo unatarajia kuvinufaisha vijiji vya Nangombo,Likwilu,Ruhekei na Kilosa vilivyopo katika mji wa Mbambabay na kwamba uwezo wa chanzo cha maji unalenga pia kufikisha huduma ya maji eneo la Mbambabay.

“Mradi utasaidia kupunguza magonjwa ya milipuko kwa jamii kutokana na kuimairika kwa huduma ya maji,jamii itapata muda wa kufanya shughuli za maendeleo’’,alisema.

Hata hivyo amesema mradi huo wa miezi sita ulitakiwa kukamilika Juni 18,2023 na kwamba utekelezaji wa mradi huo bado haujakamilika kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali  ikiwemo kuchelewa kwa msamaha wa kodi,malipo ya awali na kasi ndogo ya Mkandarasi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri amesema ,hivi sasa utekelezaji wa mradi umesimama kutokana na kuisha kwa muda wa mkataba wa Mkandarasi ambapo,serikali imemua kutekeleza mradi huo kwa kutumia wataalam wa ndani.

Amesema hivi sasa taratibu za kusitisha mkataba na Mkandarasi aliyekuwa amepewa kazi  zinaendelea na kwamba matarajio ni kwamba kazi hiyo inatarajia kutekelezwa kwa miezi nane kuanzia Juni 2024.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Kanali Ahmed Abbas amesisitiza utekelezaji wa mradi huo,kufanywa na wataalam wa ndani kwa uadilifu kwa sababu mradi umechelewa.

Amesema wananchi wanatamani kupata huduma ya maji kwa kuwa serikali imetoa mabilioni ya fedha kuhakikisha mradi huo unakamilika hivyo amewataka RUWASA kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kutekeleza mradi huo.

Baadhi ya wananchi mjini Mbambabay wameishukuru serikali kwa kutoa fedha za mradi huo ambao wamesema ukikamilika utakuwa msaada mkubwa kwa jamii kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.