Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa maji katika eneo la Londoni Sinai, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5.
Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi Estate Constructors Limited na unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 365.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mabomba ya usambazaji maji katika eneo la mradi, Kaimu Meneja wa Uendelezaji Miundombinu kutoka SOUWASA, Eng. Vicent Bahemana, alitoa onyo kali kwa wananchi dhidi ya vitendo vya wizi wa mabomba.
Alisisitiza kuwa wizi huo unaweza kusababisha baadhi ya wakazi kukosa huduma ya maji na kuathiri mafanikio ya mradi huo muhimu.
Bahemana pia aliwataka wananchi wa Sinai na Mang’ua kuwa wavumilivu wakati wa utekelezaji wa mradi, ambao unalenga kulaza mabomba yenye urefu wa kilomita 44.9.
Alieleza kuwa vipaumbele vimewekwa katika maeneo ya kijamii kama vile shule, hospitali, makanisa na misikiti ili kuhakikisha huduma ya maji inawafikia watu wote.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Lilambo, Yobo Mapunda, aliipongeza serikali kwa kuanza mradi huo na kueleza kuwa wakazi wa Sinai na Mang’ua sasa wana deni la kumpigia kura Rais Samia kutokana na utekelezaji wa ilani ya CCM.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.