Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya amezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 60 katika kijiji cha Kilimasera, kata ya Mchomoro.
Mradi huo uliahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma Septemba 2025.
“Mradi huu umekamilika, na wananchi wamefurahia kupata huduma ya maji safi na salama “,alisema Malenya.
SOUWASA imethibitisha kuwa maji yanapatikana kwenye tanki, na juhudi za kuimarisha upatikanaji wa maji zinaendelea.
Kaulimbiu ya “Kazi na Utu” inaendelea kusisitizwa kwa maendeleo endelevu kuelekea mwaka 2025-2030.
Wiki ya maji imefanyika nchini kote kuanzia Machi 16 hadi 22 mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.