MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema ametembelea miradi inayotekelezwa Halmashauri ya Madaba ikiwemo nyumba ya Kuishi Mkurugenzi pamoja na nyumba sita za watumishi.
Mgema amesema serikali imetoa shilingi bilioni tatu na milioni miasaba hamsini kwaajili ya kujenga ofisi ya Mkurugenzi kwa mara ya kwanza ilijengwa na TBA ,baadaye ilijengwa kwa force account na kuokoa shilingi milioni miasaba hamsini na kuelekezwa kujenga nyumba za watumishi
“Baada ya kutembelea miradi hii nichukue nafasi hii kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wakuu wa idara kwa kusimamia kazi hii vizuri, imefanyika kwa viwango na kwa mda mfupi ,na tumetumia milioni 270 katika nyumba ya Mkurugenzi na imefikia hatua za mwisho na milioni 350 ambazo zimetengwa katika ujenzi wa nyumba ya Mkurungenzi itaokoa kiasi Fulani cha fedha na zitatumika kwaajili ya kununulia vifaa vya ndani”.
Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Mwandishi Nchimbi amesema nyumba 6 za watumishi zimeghalimu shilingi milioni 300 kila nyumba milioni 50 na hatua iliyofikia ni nzuri na kila jengo linalojengwa tunatengemea kuokoa kiasi cha fedha na kusaidia kuweka samani za ndani za nyumba hizo.
Hata hivyo Nchimbi amesema miradi hiyo imefikia hatua ya umaliziaji na chanzo cha fedha hizo za ujenzi wa nyumba za watumishi ,fedha zilizobaki kutoka katika unjenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi iliyojengwa kwa shilingi bilioni 2.9.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda amesema Halmashauri hiyo ni changa na uwepo wa nyumba hizo zitatatua changamoto ya Makazi ya watumishi na kuongeza ufanisi katika utumishi.
Hata hivyo amesema eneo hilo limetengwa kwaajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi na kwasasa Halmashauri imepata nyumba za kuanzia 6 na tunategemea kujenga zingine ili wafanyakazi wapate mahali pazuri pakuishi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.