SERIKALI yaweka Mifumo ya Usajili wa Kamati ya Msaada wa Kisheria katika Mikoa 26.
Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geophrey Pinda alipozungumza na Kamati ya Msaada wa Kisheria Mkoa wa Ruvuma katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea.
“Serikali imeweka Mfumo unaosajili Kamati za Msaada wa Kisheria kuanzia Ngazi za Mikoa na Serikali za Mitaa”.
Pinda amesema Mfumo huo upo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria inapelekea kurahisisha utekelezaji wa Kamati hizo pamoja na kutoa huduma kwa wananchi kirahisi.
“Lengo kuu la kukutana nanyi ni kufahamiana na kutambua jitihada mnazofanya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma mnazofanya”.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo amesema Sheria namba 1 ya mwaka 2017 ya Msaada wa Kisheria pamoja na taratibu zake za mwaka 2018 hadi sasa imefika miaka mitano tangia kupitishwa na kuanza kutekelezwa.
Amesema Sheria hiyo ipo kwaajili ya kusimamia na kuratibu kwa watoa huduma wa Msaada wa Kisheria Nchini ikiwa lengo kuhakikisha wananchi wananpata huduma bure.
Mwakilishi wa Katibu wa Kamati ya Msaada wa Kisheria Mstapher Songambele amesema Kamati ya Mkoa wa Ruvuma wamefanikiwa kuwafikia watu mbalimabli ikiwemo Magereza,Wanafunzi wa Ngazi zote pamoja na Makundi maalumu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Julai 29,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.